"Kutoka shambani hadi sokoni" Kuimarisha kila hatua ya mnyororo wa thamani wa sekta ya kilimo kwa lengo la kuongeza tija, kuhakikisha ubora wa bidhaa na kuongeza kipato cha mkulima.
Pembejeo
Usambazaji wa mbegu bora, mbolea, na rasilimali nyingine kwa ajili ya uzalishaji.
Uzalishaji
Kuwawezesha wakulima kupata vifaa, ujuzi, na huduma za fedha ili kuleta tija katika uzalishaji.
Uhifadhi
Kuwezesha upatikanaji wa maghala, vihenga vya kisasa na vyumba vya barafu ili kutatua tatizo la upotevu wa mazao baada ya kuvuna na kuhakikisha ubora wa bidhaa.
Uchakataji
Kuongeza thamani ya mazao ghafi ya kilimo, mifugo na uvuvi kwa kutumia teknolojia za kisasa ili kuboresha bidhaa.
Usambazaji
Kuongeza ufanisi katika usambazaji wa bidhaa kwenye masoko kupitia njia mbali mbali za usafirishaji.
Masoko
Kuwezesha upatikanaji wa masoko mapya ya bidhaa za kilimo ili kumuongezea mkulima mapato.
Kama mteja wetu wa thamani tunakuletea bidhaa bora za kifedha zitakazokidhi mahitaji yako, kwa uzoefu wetu tutahakikisha mradi wako unawezeshwa ili kufikia malengo.
"Kuwezesha Viwanda vya Mazao ya Kilimo" Kutoa mikopo ya muda mrefu kwa ajili ya kuwezesha ujenzi wa miundombinu ya miradi ya uchakataji wa mazao itakayochochea ukuaji wa sekta ya kilimo nchini.
"Kuwezesha upatikanaji wa mitaji katika msimu husika" ili kurahisisha utendaji kazi katika hatua mbalimbali za mnyororo wa thamani kuanzia kupanda hadi kuuza kwa mlaji wa mwisho.