Skip to main content

Maswali Yanayoulizwa Zaidi

Naweza kufanya nini kupitia mikopo ya Asset Finance?

Unaweza kufanya ununuzi wa matrekta, mashine za kupanda, kuvuna, mifumo ya umwagiliaji, teknolojia za baada ya mavuno (kama maghala na silos), mashine za kuongeza thamani na magari ya usafirishaji wa kilimo.

Naweza kupata kiwango gani cha mkopo?

Hadi 75% ya gharama ya mali, kutegemea uhalali wa mradi.

Muda wa marejesho ni upi?

Hadi mwaka 1, ukilipwa kwa awamu kulingana na mtiririko wa mapato.

Je mkopo wa Project Finance unalenga nini?

Inawezesha ununuzi wa miundombinu ya muda mrefu ya kilimo kama skimu za umwagiliaji, maghala ya kisasa, viwanda vya usindikaji na vituo vya masoko.

Muda wa juu wa mkopo ni upi?

Kati ya mwaka 1 hadi miaka 15, kutegemea mradi.

Nani anastahili?

Wakulima wadogo, SME’s, vyama vya ushirika, wafugaji na waendesha biashara za kilimo.

Mkopo wa msimu (Term Loan) unatumiwa kwa nini?

Kuwezesha shughuli za msimu kama kuandaa shamba, kununua mbegu na mbolea, chakula cha mifugo, na mavuno.

Riba ni kiasi gani?

Wakulima wadogo: 8% – 12% na - Wakulima wa kati na wakubwa: 13% – 15%

Muda wa mkopo ni upi?

Miaka 1–3

Malipo ya Bima (Insurance Premium Finance – IPF) inafadhili nini?

Malipo ya bima zisizo za maisha kama bima ya mali, bima ya kilimo, bima ya magari na bima ya maisha ya mkopo.

Muda wa marejesho ni upi?

Kawaida hadi miezi 10, na si zaidi ya miezi 12 katika mazingira maalum.

 

Nani anaweza kuomba?

Mchezaji yeyote katika mnyororo wa thamani wa kilimo mwenye wajibu wa kulipa bima.

Ni huduma gani inatolewa kwa ajili ya Mikopo ya Biashara na Bidhaa (Trade & Commodity Finance)?

Mikopo ya uagizaji/uasafirishaji, mkopo wa kabla na baada ya usafirishaji, punguzo la ankara, barua za mkopo na ufadhili wa bidhaa.

Muda wa mkopo ni upi?

Miaka 5–15, kulingana na mpango.

Riba ni kiasi gani?

Kati ya 8% hadi 15% kwa mwaka.

Dhamana ya Mikopo kwa Wakulima Wadogo (Smallholder Credit Guarantee Scheme – SCGS)ni nini?

Ni mpango ambapo TADB inashiriki hatari ya mikopo inayotolewa na benki washirika kwa wakulima wadogo, kuwasaidia kupata mikopo bila dhamana kamili.

Inafadhili nini?

Vifaa vya shambani, mashine, mifumo ya umwagiliaji, mifugo bora na miundombinu ya shamba.

Dhamana hudumu kwa muda gani?

Inategemea makubaliano kati ya TADB na benki shiriki.