Sera za Faragha
Tarehe ya Kuanza Kutumika: Jan 2025
1. Utangulizi
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (“TADB”, “sisi”, “yetu” au “benki”) imejitolea kulinda faragha na usiri wa taarifa za watumiaji (“wewe” au “yako”) wanaotembelea au kushirikiana na tovuti yetu www.tadb.co.tz (“Tovuti”). Sera hii ya Faragha inaeleza jinsi tunavyokusanya, kutumia, kufichua, kuhifadhi, na kulinda data yako binafsi unapoutumia tovuti wetu.
Kwa kutumia tovuti hii, unakubaliana na ukusanyaji na matumizi ya taarifa zako kulingana na masharti ya Sera hii.
2. Wigo na Utekelezaji
Sera hii inawahusu watembeleaji wote, wateja, washirika, na watumiaji wa tovuti (ikiwemo kupitia wavuti, simu, au mifumo mingine). Inahusu data binafsi inayokusanywa kupitia tovuti, lakini haitumiki kwa data zinazokusanywa nje ya mtandao au kupitia huduma za wahusika wengine zisizo chini ya TADB.
Iwapo kutakuwa na mgongano kati ya sera hii na sheria yoyote inayotumika, sheria husika ndiyo itakayochukua nafasi.
3. Aina za Taarifa Tunazokusanya
a) Taarifa Binafsi Unazotoa
- Jina, anwani, barua pepe, na namba ya simu
- Namba ya utambulisho au usajili wa biashara
- Maombi, maswali, maoni au mawasiliano unayotuma kwetu
- Taarifa nyingine unazotoa kwa hiari (kama kwenye fomu, tafiti, au maombi ya mawasiliano)
b) Taarifa Zinazokusanywa Kiotomatiki
- Anwani ya IP
- Aina na toleo la kivinjari, mfumo wa uendeshaji
- Kurasa ulizotembelea, muda uliotumia, na tovuti ulipotoka
- Vitambulisho vya kifaa na eneo la kijiografia (takriban)
- Data za vidakuzi (cookies) na teknolojia za ufuatiliaji
c) Data Kutoka kwa Watoa Huduma Wengine
- Watoa huduma za uchambuzi (mfano: Google Analytics)
- Huduma za matangazo au ufuatiliaji wa maslahi
- Mitandao ya kijamii au majukwaa mengine ya nje unaposhirikiana nayo
4. Matumizi ya Taarifa
Tunaweza kutumia taarifa zako kwa madhumuni yafuatayo:
- Kutoa na kuendesha huduma za tovuti
- Kujibu maswali, maombi au malalamiko
- Kukutumia taarifa muhimu (kama mabadiliko ya sera au masharti)
- Kuchambua matumizi ya tovuti na kuboresha huduma
- wa matangazo au taarifa za masoko (kwa ridhaa yako)
- Kubinafsisha maudhui na kuonyesha matangazo husika (kwa ridhaa yako)
- Kugundua na kuzuia udanganyifu au shughuli zisizoidhinishwa
- Kutii matakwa ya kisheria na sera za ndani
5. Vidakuzi na Teknolojia za Ufuatiliaji
Sisi na watoa huduma wa nje tunatumia vidakuzi (cookies), alama za wavuti (web beacons), na teknolojia sawa kukusanya taarifa za matumizi na mapendeleo.
- Unaweza kutoa ridhaa yako kupitia mipangilio ya faragha ya tovuti.
- Unaweza kubadilisha au kuondoa ridhaa yako wakati wowote kupitia ikoni ya mipangilio (kwa kawaida upande wa kushoto wa ukurasa).
- Kwa maelezo zaidi kuhusu aina za vidakuzi, muda wake na jinsi ya kuvizima, tafadhali tembelea ukurasa wetu wa Sera ya Vidakuzi.
6. Msingi wa Kisheria wa Kuchakata Data
Kulingana na sheria, tunachakata data zako binafsi ikiwa tu kuna msingi halali, ikiwemo:
- Ridhaa yako
- Utekelezaji wa mkataba au hatua kabla ya kuingia mkataba
- Wajibu wa kisheria au wa udhibiti
- Maslahi halali ya TADB (kwa sharti kuwa hayapingani na haki zako).
7. Kushiriki na Kufichua Taarifa
Hatuziuzi au kukodisha data zako binafsi. Hata hivyo, tunaweza kushiriki taarifa zako katika hali zifuatazo:
- Kwa watoa huduma, wakandarasi au wasambazaji wanaosaidia kuendesha tovuti (chini ya makubaliano ya usiri)
- Kwa mamlaka za kiserikali au udhibiti, pale inapohitajika kisheria
- Kutekeleza masharti yetu au kulinda haki, usalama, au mali
- Wakati wa muunganiko, ununuzi au mabadiliko ya kiutawala (kwa masharti ya ulinzi wa data).
8. Uhifadhi wa Data
Tutahifadhi data zako binafsi kwa muda unaohitajika kwa madhumuni yaliyokusudiwa au kutimiza matakwa ya kisheria na uhasibu. Baada ya muda huo, data zako zitafutwa au kufanywa zisizotambulika kwa njia salama.
9. Usalama wa Data
Tunatekeleza hatua za kiufundi na kiutawala kulinda data zako dhidi ya ufikiaji, ufunuo, mabadiliko au uharibifu usioidhinishwa. Hatua hizi ni pamoja na udhibiti wa ufikiaji, usimbaji wa taarifa (encryption), ufuatiliaji, na mafunzo kwa wafanyakazi.
Hata hivyo, njia yoyote ya usafirishaji wa data kupitia mtandao si salama kabisa, hivyo hatuwezi kuhakikisha usalama wa asilimia mia moja.
10. Haki Zako
Kulingana na sheria husika, unaweza kuwa na haki zifuatazo:
- Haki ya kupata taarifa zako
- Haki ya kusahihisha, kusasisha, au kufuta taarifa zako
- Haki ya kupinga au kuzuia uchakataji wa data
- Haki ya kuhamisha data zako
- Haki ya kuondoa ridhaa wakati wowote (ikiwa uchakataji unategemea ridhaa)
- Haki ya kuwasilisha malalamiko kwa mamlaka ya usimamizi.
Ikiwa ungependa kutumia haki hizi, tafadhali wasiliana nasi kupitia sehemu ya “Wasiliana Nasi” hapa chini.
11. Watoto na Vijana Wadogo
Tovuti yetu haielekezwi kwa watoto walio chini ya umri wa miaka 18. Hatukusanyi kwa makusudi data kutoka kwa watoto walio chini ya umri huo. Iwapo unaamini tumekusanya taarifa za mtoto, tafadhali wasiliana nasi ili tuzifute.
12. Viungo vya Wavuti za Watu Wengine
Tovuti inaweza kuwa na viungo vya tovuti, programu, au huduma za wahusika wengine. Hatutawajibika kwa sera za faragha au maudhui ya tovuti hizo. Tunashauri usome sera zao za faragha kabla ya kushirikiana nazo.
13. Mabadiliko ya Sera Hii
Tunaweza kusasisha Sera hii ya Faragha mara kwa mara. Tukifanya mabadiliko makubwa, tutawaarifu watumiaji kwa kuweka toleo jipya kwenye tovuti lenye tarehe ya utekelezaji. Kuendelea kutumia tovuti baada ya mabadiliko kutamaanisha umekubali sera mpya.
14. Wasiliana Nasi
Iwapo una maswali, wasiwasi, au maombi yanayohusiana na Sera hii ya Faragha au usimamizi wa data zako binafsi, tafadhali wasiliana nasi kupitia:
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB)
Kiwanja Na. 84K | Acacia Estates
S.L.P. 63372, Dar es Salaam
Barabara ya Kinondoni
Barua pepe: info@tadb.co.tz
Simu: +255 222 923 500