Utaratibu wa kuwasilisha na kushughulikia malalamiko
Je umeridhika na huduma zetu?
Utaratibu wa kuwasilisha na kushughulikia malalamiko
Tunu za benki ya Maendeleo ya Kilimo ni Uaminifu na Taaluma unaozingatia huduma kwa mteja. Hivyo, siku zote, ni azma yetu kumweka mteja mbele. Hata hivyo, tunatambua ya kwamba inaweza ikatokea kwamba haujaridhika na huduma zetu, au hatujatimiza matarajio yako. Kama ni hivyo, unaweza kuwasilisha malalamiko yako kwa mpangilio ifuatayo:
- Onana na Meneja wa Kanda na wasilisha malalamiko yako kwa mdomo ama kwa maandishi.
- Jaza fomu ya malalamiko na kuiwasilisha mapokezi au kuitumbukiza kwenye Sanduku la Maoni lililoko ofisi za kanda.
- Tuma barua pepe kwenda: complaints@tadb.co.tz
Tuma barua pepe moja kwa moja kwa Maafisa Waandamizi wafuatao
Meneja Mawasiliano publicrelations@tadb.co.tz
Mkurugenzi wa Biashara directorbusiness@tadb.co.tz
Mkurugenzi Mtendaji md@tadb.co.tz- S.L.P 63372, Dar es Salaam, Tanzania
- Namba za Simu: 0800 110 120 au +255 22 292 3501/2
- Jaza fomu ya maoni kwenye tovuti yetu www.tadb.co.tz
- Tuma ujumbe kupitia mitandao yetu ya kijamii (Twitter, Instagram and Facebook) @tadbtz
- Kujaza fomu maalum ya usajili wa malalamiko ya wateja kinachopatikana tawini na kwenye tovuti yetu www.tadb.co.tz
Ni azma yetu kushughulikia malalamiko yako kadri tutakavyo yapokea na utapewa mrejesho juu ya hatua zilizochukuliwa ndani ya siku 10 za kazi.
Ikiwa hautaridhika na hatua hizo, unaweza kuwasilisha malalamiko yako, kwa kujaza fomu maalum (Fomu Na. 1) inayopatikana tawini, na kuituma ama kupitia barua pepe, kuipeleka mwenyewe, kwa posta, au tarakishi, kwenda Dawati la Kushughulikia Malalamiko lililoko Benki Kuu ya Tanzania kwa anuani ifuatayo:
Dawati la Kushughulikia Malalamiko,
Ofisi ya Mwanasheria wa Benki, Benki Kuu ya Tanzania,
2 Mtaa wa Mirambo Barabara ya 40184,
Dar es Salaam, Tanzania,
S.L.P.2939.
Simu: +255 26 2963183/7 or +255 22 2232506
Tarakishi: +255 26 2963189