ORODHA YA HATI/TAARIFA INAYOTAKIWA KWA UOMBI WA MIKOPO.
- Mamlaka ya kukopa
- Azimio la Bodi linaloruhusu kukopa.
- Barua ya maombi ya mkopo inayoonyesha aina na kiasi cha mkopo kinaohitajika, madhumuni ya mkopo, chanzo cha marejesho na muda wa marejesho.
- Uhalali wa mkopaji
- Cheti cha usajili
- Katiba na kanuni za uendeshaji
Leseni halali ya biashara. - Namba ya utambulisho wa mlipakodi (Cheti cha TIN).
- Cheti cha uthibitisho wa malipo ya kodi.
- Cheti cha usajili wa kodi ya ongezeko la thamani (VAT).
- Vibali kutoka mamlaka husika (kama vile, TFDA, TBS).
- Taarifa za mwaka za hivi karibuni zilizowasilishwa kwa msajili wa makampuni.
- Uendeshaji wa biashara
- Mpango wa biashara.
- Taarifa za fedha zilizokaguliwa kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita. Taarifa za mahesabu zionyeshe mwenendo na mabadiliko katika biashara pamoja na ripoti ya Mkurugenzi.
- Taarifa za fedha za muda za hivi karibuni (Taarifa za Uongozi).
- Makadirio ya baadae ya mzunguko wa fedha.
- Taarifa ya akiba ya bidhaa na wadaiwa wa bidhaa (kwa kuzingatia umri).
- Taarifa za uhusiano wa mkopaji na benki wa sasa na uliopita pamoja na historia yake ya ukopaji (Vigezo na masharti ya mikopo aliyo nayo kutoka benki nyingine).
- Taarifa ya akaunti ya mkopaji kwa miezi 12 iliyopita.
- Historia ya kampuni, kuhusu umiliki, na uzoefu wa viongozi wakuu ikihusisha taaluma zao na uzoefu katika nafasi zao (wasifu wao- CVs).za Wakurugenzi na Timu ya Uongozi zinazoonyesha sifa na uzoefu.
- Nakala za vitambulisho vya wakurugenzi (Kitambulisho cha Mpiga Kura au Kitambulisho cha Taifa).
- Orodha ya wanunuzi na wauzaji wakuu pamoja na makubaliano yenu ya kibiashara.
- Mikataba ya biashara (makubaliano yaliyosainiwa kati ya mkopaji na wanunuzi wa bidhaa au wauzaji wa pembejeo).
- Ankara ya malipo (Proforma Invoice) mtambo/vifaa/mashine itakayowezeshwa (kwa mkopo wa ununuzi wa mtambo/vifaa/mashine).
- Orodha ya akiba ya mali/bidhaa iliyohakikiwa.
- Dhamana ya mkopo.
- Nakala za hati ya dhamana inayopendekezwa kwa ajili ya mkopo.
- Tathmini ya awali ya dhamana inazopendekezwa.