Biashara
TADB inatoa huduma za fedha zilizobuniwa kukidhi mahitaji mbalimbali ya sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi nchini Tanzania.
Mikopo yetu imegawanyika katika makundi makuu mawili ambayo ni (i)Mikopo ya Moja kwa Moja inayowaruhusu wateja kukopa moja kwa moja kutoka TADB kupitia huduma mbalimbali za fedha na (ii) Mikopo isiyo ya Moja kwa Moja inayowaruhusu wateja kukopeshwa na TADB kupitia taasisi shiriki za fedha. Aidha, huduma za mikopo zinazotolewa kwa njia isiyo ya moja kwa moja ni pamoja na mfuko wa dhamana wa wakulima wadogo; na mikopo ya jumla kwa taasisi za fedha.