Bidhaa hii ni dhamana ya mtu binafsi au dhamana ya mkoba inayosimamiwa na TADB kwa ajili ya mikopo ya kilimo inayotolewa kwa wakulima wadogo na benki shiriki. Dhamana hii inalenga kupunguza hatari ya mikopo inayotolewa katika sekta ya kilimo. Bidhaa hii itasaidia kutatua changamoto ya ufadhili mdogo (kwa watu binafsi, SME na taasisi) katika sekta ya kilimo kutokana na ukosefu wa dhamana ya kutosha na taasisi nyingine za kifedha kushindwa kutoa mikopo kwa vikundi vya wakulima wadogo. Matokeo yake, wanufaika wa mikopo hii wataweza kupata vifaa vya kilimo, pembejeo za kilimo (mbegu bora, mifugo ya kuzalisha, mbolea na viuatilifu), vifaa vya umwagiliaji na miundombinu mingine ya shamba, na hivyo kubadilisha sekta hii na kuongeza mchango wake katika ukuaji wa uchumi.