Skip to main content

Kuhusu Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania

Kuhusu Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania

Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) ni taasisi ya kifedha ya maendeleo, iliyoanzishwa chini ya sheria ya makampuni ya mwaka 2002 kisha kusajiliwa chini ya sheria ya mabenki na taasisi za fedha Na. 5 ya mwaka 2006 kwa lengo la kutoa mikopo ya muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu ili kuleta mapinduzi ya  sekta ya kilimo nchini Tanzania.

Dira

Kuwa taasisi ya kifedha ya maendeleo inayoongoza katika kuleta mapinduzi ya kilimo nchini.

Dhima

Kuchangia usalama wa chakula na  kupunguza umaskini kwa kuchagiza mapinduzi ya kilimo kupitia huduma bunifu za mikopo zinazoendeleza minyororo ya thamani ya kilimo jumuishi na endelevu.

Tunu za Msingi

  • Uadilifu – Kudumisha uwazi, uwajibikaji, na viwango vya juu vya maadili.
  • Kujifunza na Ubunifu - Kuchochea ubunifu endelevu na imara.
  • Weledi - Kufanya kazi kwa kuzingatia ujuzi, maarifa, na viwango vya kitaalamu.   
  • Kufanya kazi kama timu - Kushirikiana kwa ufanisi ili kufikia malengo ya pamoja. 
  • Mitizamo Tofauti na Ushirikishwaji - Kuheshimu na kuthamini mawazo, mitizamo na ushiriki wa watu wote.

Malengo Makuu

  1. Kuchangia katika utoshelevu na usalama wa chakula. 
  2. Kuleta mapinduzi ya kilimo kutoka kilimo cha kujikimu kwenda kilimo cha kibiashara kitakachochangia ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini.

Vipaumbele (Maeneo ya kuleta Matokeo)

  1. Kuchagiza upatikanaji wa mikopo kwenye sekta ya kilimo - Kuwa taasisi ya kifedha ya maendeleo inayoongoza na kuchagiza taasisi nyingine za fedha kuongeza mikopo katika sekta ya kilimo.
  2. Kuendeleza Minyororo ya Thamani – (i)Kuwezesha uwekezaji katika miundombinu ya uzalishaji, mitambo, vifaa vya uhifadhi, uchakataji, usafirishaji, biashara ya mazao na(iii) kuhamasisha biashara miongoni mwa wakulima wadogo.
  3. Mabadiliko ya Tabia Nchi na Kilimo kinachokabiliana na mabadiliko ya tabia nchi - Kuwawezesha wakulima wadogo, vyama vya ushirika makampuni ya kilimo kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
  4. Huduma za fedha jumuishi - Kuwezesha upatikanaji wa mikopo ya kilimo, vifaa vya uzalishaji na masoko kwa wanawake na vijana wanaojishughulisha na kilimo biashara.
  5. Uwezo wa Kutoa Huduma – (i)Kuendeleza mahusiano ya kitaasisi na utafutaji wa rasilimali fedha kwa ajili ya kukopesha kwenye sekta ya kilimo; na (ii) Kuimarisha uwezo na kutanua wigo wa TADB kutoa huduma kwa kuwekeza kwenye watu na mifumo ili kuimarisha ufanisi, utawala pamoja na usimamizi wa ukidhi wa viashiria.