Huu ni ufadhili wa muda mrefu wa miundombinu na miradi ya viwanda unaotegemea makadirio ya mtiririko wa fedha wa mradi pamoja na Taarifa za Kifedha za awali za mdhamini.
Unakusudiwa kufadhili mahitaji ya miundombinu ya mnyororo wa thamani wa kilimo kama vile ujenzi wa miradi ya umwagiliaji, maghala ya kisasa ya kuhifadhia mazao, vituo vya masoko na mahitaji mengine ya mikopo ya miundombinu ya kilimo kwa ajili ya kujenga na kuimarisha minyororo ya thamani ya kilimo. Mkopo unalipwa kulingana na mpango wa malipo, mtiririko wa fedha wa mradi, na kulingana na aina ya mkopo kama vile mkopo wa muda mfupi, mkopo wa muda wa kati au mkopo wa muda mrefu. Ulipaji wa mkopo unafanyika kwa awamu na kwa kuzingatia muda wa kurejesha mkopo.