TADB NA PASS WAINGIA MAKUBALIANO YA KUWEKEZA KWA WAJASIRIAMALI WADOGO

TADB imeingia makubaliano na Private Agricultural Sector Support Trust (PASS) ambayo ni shirika lililoanzishwa mwaka wa 2000 kwa lengo la kukuza, maendeleo na ukuaji wa kilimobiashara kwa ajili ya ujasiriamali wadogo wa kilimobiashara. Makubaliano haya ni katika kuwekeza na kukuza miradi ya ubunifu ya kilimo kwa wanawake, vijana na wajasiriamali wadogo, kupitia programu ya kuwajengea uwezo, kubuni, kuwezesha na kukuza miradi hiyo ya kilimo kwa kutumia na ujuzi kutoka kwa (TADB) na (PASS).

Zaidi ya watu 19,250,000 nchini Tanzania ni vijana kati ya miaka 15 hadi 35, na kati ya hao, vijana 800,000 wanahitimu vyuo vikuu na taasisi ya elimu ya juu kila mwaka na kulifanya soko la ajira kufurika zaidi licha tayari limeshajaa vijana wasiokuwa na ajira, ingawa vijana wengi wanahitimu wakiwa na mawazo ya kibunifu katika sekta mbalimbali. Mpaka sasa TADB imeshatoa bilioni 147 kwa miradi ya kilimo takriban 153, na katika jukumu la TADB katika kuchagiza maendeleo ya kilimo, na kwa makubaliano haya ya kuatamiza na kuwekeza katika miradi ya ubinifu wa kilimo kwa vijana, TADB itashiriki katika fedha tatizo la ajira na itapata fursa kubwa ya kutoa huduma kwa kundi hili kubwa la vijana na wanawake na kujifunza zaidi changamoto katika miradi ya kilimo ya ubunifu ambayo kikundi hiki hufaamika zaidi kama nguvu kazi ya nchi.

TADB itaendelea kuchagiza kuweka la kuweka na kuyapa thamani ya kilimo kwa vijana, wanawake na wajasiriamali wadogo kwa kupata mikopo na huduma mbalimbali za kifedha pamoja na kuwakutanisha na kuomba wakubwa katika sekta ya kilimo.

Na kwa pia na PASS ambao tayari wameshaanza kuamiza miradi ya vijana chao cha ubunifu katika Kilimo biashara (Agribusiness Innovation center) kilichoanzishwa mwaka 2015 kinachotoa huduma za biashara zinazolenga kutatua changamoto za biashara za kilimo. Kituo cha kwanza ki kukusanya pamoja na chuo kikuu cha kilimo cha SUA, mkoani Morogoro kwa ajili ya kilimo cha mboga, mapato na kilimo cha samaki mwezi uliopita vijana 20 walimaliza mafunzo na wanatarajia kunufaika na TADB kupitia makubaliano haya. Kituo kingine kimewekwa kwa ajili ya kuuza bidhaa za mifugo na nyama. TADB itashiriki kuongea atamiza (Incubators) hizi ili kuwafikia vijana, wanawake na wajasiriamali wadogo na kutoa fursa nyingi kwa benki katika huduma mbali mbali za kifedha hususani mfuko wa dhamana kwa wakulima (SCGS) ambapo miradi ya vijana, wanawake na wajasiriamali wengi watafaidika na mfuko huu wa dhamana.

PASS amekuwa mdau mkuu wa TADB na sekta nzima ya kilimo ambao ni dhamana ya mikopo kati ya 20% hadi 60% kwa jumla ya wakulima binafsi 929,102 na jumla ya mikopo ni bilioni 712 kati yam waka 2000 hadi 2018.

Tunaamini kwamba makubaliano haya yatahakikisha miradi hii ya ubunifu inaleta maendeleo chanya katika jamii na nchi kwa ujumla na Lengo ni kuwekeza na kuwawezesha vijana zaidi ya 500 kwa mwaka ambao asilimia 50% watakuwa wanawake.