-
TADB yatoa Mafunzo kwa Wakulima Viziwi
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imeonyesha kwa vitendo nia yake ya kuinua wakulima wadogo wa makundi maalum nchini kwa kufanya mafunzo ya siku 3 kwa Kituo cha Wakulima Wafugaji Viziwi Tanzania (KIWAWAVITA) yaliyoandaliwa na TADB katika katika ukumbi wa Edema, mkoani Morogoro.
Mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo kwa nadharia na vitendo wakulima hao wa kituo hicho cha Wakulima na Wafugaji Viziwi Tanzania ili wainuke kiuchumi na kuongeza uzalishaji wa tija.
Mafunzo hayo yalijumuisha mada kama:
📖 Elimu ya Fedha na Biashara
🌾 Huduma zinazotolewa na TADB
👨🌾 Kilimo cha Mbogamboga
🥑 Kilimo cha Kisasa
Mafunzo hayo ni muendelezo wa mpango wa TADB katika kufikia wakulima wa makundi maalum ili kuwajengea uwezo wakulima wadogo nchini waweze kutoka katika kilimo cha kujikimu kwenda kwenye kilimo cha kibiashara. -
TADB ni mwanga wa maendeleo ya wafugaji
Ahsante CAN BE FARMING Ltd. kwa ushuhuda huu mzuri. Kama Benki ya kimaendeleo, tunajivunia kuwa sehemu ya safari yako kibiashara.
Je wewe ni mkulima, mfugaji, au mvuvi na ungependelea kuendeleza mradi wako kupitia TADB?
Wasiliana nasi.
#WikiYaHudumaKwaWateja
#SheherekeaHuduma -
Tunaishukuru TADB kwa mchango wao kwenye Kilimo
#WikiYaHudumaKwaWateja
Sikiliza simulizi kutoka mteja wetu, Great Farm, kuhusu namna TADB tulivyoweza kuleta mageuzi katika ufugaji wao wa kuku wa mayai, kutoka kuku elfu 30 hadi laki 120.
Hakika #KilimoKinaBenkika
#SheherekeaHuduma -
TADB yatoa elimu kwa Wafugaji wadogo
Moja ya malengo yetu kama benki ni kumwezesha mkulima kutoka kilimo cha kujikimu kwenda kwenye kilimo cha biashara.
Pamoja na mikopo ya riba nafuu tunayotoa, TADB tunatambua umuhimu wa utolewaji wa elimu ya kifedha kwa ajili ya kuwezesha lengo hili.
Hii ni simulizi ya wafugaji wadogo kutoka vyama vya wafugaji vya mkoa wa Kilimanjaro waliofaidika na mafunzo ya elimu ya kifedha na ushirika kutoka TADB hivi karibuni.
#Kilimokinabenkika -
TADB na Sekta ya Maziwa
Sekta ya Maziwa nchini inachangia kadiri ya 1.5% katika pato la Taifa. Nchi jirani kama vile Kenya na Rwanda, sekta hii inachangia hadi kiasi cha asilimia 6 ya pato la mataifa haya. Serikali inachukua hatua mbalimbali za kuiwezesha sekta hii kuongeza tija.
#KilimoKinaBenkika #tadb #Benkiyamaendeleoyakilimo -
Zana Bora kwa kilimo chenye tija
MEDIA GALLERY
Click through our media gallery to view photos and related media of our engagements with farmers, partners and other stakeholders.