TADB NA PASS WAINGIA MAKUBALIANO YA KUWEKEZA KWA WAJASIRIAMALI WADOGO

TADB imeingia makubaliano na Private Agricultural Sector Support Trust (PASS) ambayo ni shirika iliyoanzishwa mwaka 2000 kwa lengo la kuongeza uwekezaji, maendeleo na ukuaji wa kilimobiashara kwa ajili ya wajasiriamali wadogo wa kilimobiashara. Makubaliano haya ni katika kuwekeza na kukuza miradi ya ubunifu ya kilimo kwa wanawake, vijana na wajasiriamali wadogo, kupitia programu ya kuwajengea uwezo, kubuni, kuwezesha na kukuza miradi hiyo ya kilimo kwa kutumia rasilimali na ujuzi kutoka kwa (TADB) na (PASS).

Zaidi ya watu 19,250,000 nchini Tanzania ni vijana kati ya miaka 15 hadi 35, na kati ya hao, vijana 800,000 wanahitimu vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu kila mwaka na kulifanya soko la ajira kufurika zaidi licha tayari limeshajaa vijana wasiokuwa na ajira, ingawa vijana wengi wanahitimu wakiwa na mawazo ya kibunifu katika sekta mbalimbali. Mpaka sasa TADB imeshatoa billion 147 kwa miradi ya kilimo takribani 153, na katika kuendelea na jukumu la TADB katika kuchagiza maendeleo ya kilimo, na kwa kupitia makubaliano haya ya kuatamiza na kuwekeza katika miradi ya ubinifu ya kilimo kwa vijana, TADB itashiriki katika kupunguza tatizo la ajira na itapata fursa kubwa ya kutoa huduma kwa kundi hili kubwa la vijana na wanawake na kujifunza juu ya changamoto zaidi katika miradi ya kilimo ya ubunifu ambalo kundi hili hufaamika zaidi kama nguvu kazi ya nchi.

TADB itaendelea kuchagiza ongezeko la uzalishaji na kuyapa thamani mazao ya kilimo kwa kwa vijana, wanawake na wajasiriamali wadogo kwa kupitia mikopo na huduma mbalimbali za kifedha pamoja na kuwakutanisha na wawekezaji wakubwa katika sekta ya kilimo.

Na kwa kushirikiana na PASS ambao tayari wameshaanza kuatamiza miradi ya vijana kupitia kituo chao cha ubunifu katika Kilimo biashara (Agribusiness Innovation centre) kilichoanzishwa mwaka 2015 kinachotoa huduma za kukuza biashara zinazolenga kutatua changamoto za soko kwa biashara za kilimo. Kituo cha kwanza kilianzishwa pamoja na chuo Kikuu cha kilimo cha SUA, mkoani Morogoro kwa ajili ya kilimo cha mbogamoga, usindikaji mazao na kilimo cha samaki ambapo mwezi uliopita vijana 20 walimaliza mafunzo na wanatarajia kunufaika na TADB kupitia makubaliano haya. Kituo kingine kipo Kongwa kwa ajili ya usindikaji wa bidhaa za mifugo na nyama. TADB itashiriki kuongeza atamiza (Incubators) hizi ili kuwafikia vijana, wanawake na wajasiriamali wadogo na kufungua fursa nyingi kwa benki katika kutoa huduma mbalimbali za kifedha hususani mfuko wa dhamana kwa wakulima wadogo (SCGS) ambapo miradi ya vijana, wanawake na wajasiriamali wadogo wengi watafaidika na mfuko huu wa dhamana.

PASS amekuwa mdau mkuu wa TADB na sekta nzima ya kilimo ambao hutoa dhamana ya mikopo kati ya 20% hadi 60% kwa jumla ya wakulima binafsi 929,102 na jumla ya mikopo ni billion 712 kati yam waka 2000 hadi 2018.

Tunaamini kwamba makubaliano haya yatahakikisha miradi hii ya ubunifu inaleta maendeleo chanya katika jamii na nchi kwa ujumla na Lengo ni kuwekeza na kuwawezesha vijana zaidi ya 500 kwa mwaka ambao asilimia 50% watakuwa wanawake.