TADB inapata Euro milioni 80 kutoka AFD ili kupanua ufadhili wa kilimo kwa wakulima

Katika kuimarisha shughuli zake za kutoa mikopo ya muda mfupi na mrefu katika sekta ya kilimo nchini TADB ilipata Euro milioni 80 (Tsh. 210 bilioni), kutoka Shirika la Maendeleo la Ufaransa (afd_france).

Euro Milioni 80 zitatumika katika kutatua changamoto zinazowakabili watendaji wa sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi katika kupata mitaji.

Mkataba huo umesainiwa na Mkurugenzi Mkuu wa TADB, Bw. Frank Nyabundege na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa Bw. Rioux Remy, Mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Hafla hiyo ilifanyika katika jiji la Brest nchini Ufaransa mnamo Februari 11, 2022.