TADB yatoa mafunzo kwa wakulima viziwi

Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imeonyesha kwa vitendo nia ya kuinua wakulima wadogowadogo maalumu nchini kwa mafunzo ya siku 3 kwa Kituo cha Wakulima Wafugaji Viziwi Tanzania (KIWAWAVITA) yaliyofanyika mkoani Morogoro.

Mafunzo hayo yalilenga kuwajengea uwezo wa nadharia na vitendo wakulima hao ili wainuke uchumi, kuongeza na tija katika kilimo.

Mafunzo hayo yalijumuisha mada kama:

? Elimu ya fedha na biashara ?? Kilimo cha bustani na mbogamboga ? Kilimo cha kisasa