
Wafanyakazi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) waliungana na maelfu ya Watanzania kuadhimisha Siku ya Wafanyakazi Duniani Mei 1, 2022.

Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ilihusu kuiomba serikali nyongeza ya mishahara na uboreshaji wa maslahi ya wafanyakazi wakati kazi ikiendelea.

Mkurugenzi Mtendaji Frank Nyabundege alisema maadhimisho ya siku ya wafanyakazi kwa mwaka huu ni ya sita kwa TADB kushiriki tangu kuanzishwa kwake na katika kipindi hiki kumekuwa na uboreshaji wa haraka katika taasisi hiyo ikiwa ni pamoja na ongezeko la watumishi na ufanisi katika utekelezaji wa shughuli za benki hiyo.
"Siku hii ni muhimu kwetu sote, wafanyakazi wa TABD, na wafanyakazi wote duniani kote kwa sababu inatukumbusha wajibu wetu wa kuwatumikia wananchi kwa uadilifu, umoja, ufanisi na haki zinazostahiki," aliongeza.
Nyabundege pia amewataka wafanyakazi wa TADB kuzingatia dhamira na ufanisi wao kazini ili kuleta matokeo chanya.

