KATIBU MKUU KILIMO ARIDHISHWA NA SKIMU YA UMWAGILIAJI MVUMI KILOSA

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya amesema ameridhishwa na hatua ya ujenzi wa skimu ya umwagiliaji kijiji cha Mvumi wilaya ya Kilosa ambayo imefikia asilimia 94 ya ujenzi na tayari wakulima wameanza kunufaika.

Ametoa kauli hiyo alipofanya ziara ya kushtukiza kukagua maendeleo ya mradi huo uliopo wilaya ya Kilosa Mkoa wa Morogoro chini ya mradi wa Kuongeza Tija na uzalishaji wa zao la Mpunga (ERPP).Katibu Mkuu huyo alisema mradi wa umwagiliaji kijiji cha Mvumi umegharimu shilingi Bilioni 1.97 na utanufaisha wakulima wengi wa zao la mpunga katika wilaya ya Kilosa kuongeza uzalishaji na tija.

Source – Ministry of Agriculture , Tanzania