TADB Yaadhimisha Siku ya Wanahabari; Televisheni ya Mchongo Imezinduliwa Rasmi kupitia StarTimes Chaneli 134
Uzinduzi rasmi wa Televisheni ya Mchongo kwenye king'amuzi cha StarTimes Channel 134 ni hatua muhimu katika sekta ya kilimo nchini Tanzania. Televisheni ya Mchongo ni chaneli ya kwanza na pekee inayojishughulisha na kilimo, uvuvi, ufugaji na sekta zinazohusiana katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati. Tukio hili muhimu limefanyika katika Makao Makuu ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania...
TADB yatoa mafunzo kwa wakulima viziwi
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imeonyesha kwa vitendo nia ya kuinua wakulima wadogowadogo maalumu nchini kwa mafunzo ya siku 3 kwa Kituo cha Wakulima Wafugaji Viziwi Tanzania (KIWAWAVITA) yaliyofanyika mkoani Morogoro. Mafunzo hayo yalilenga kuwajengea uwezo kwa nadharia na vitendo wakulima hao ili wainuke kuchangia, kuongeza na tija...