TADB inaadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake #IWD2025

Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania imeungana na maelfu ya wanawake duniani kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake #IWD2025 kuanzia tarehe 7 hadi 8 Machi 2025.


Maadhimisho hayo yalizinduliwa rasmi na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. David Nghambi, tarehe 7 Machi katika makao makuu ya TADB. Katika hotuba yake ya ufunguzi Bw.David, anatambua nafasi & juhudi za wanawake katika kuongeza thamani na ukuaji wa benki na maisha kwa ujumla pamoja na kukata keki kuashiria sherehe hizo.

Kilele cha #IWD2025 ni Machi 8, ambayo huadhimishwa ulimwenguni kote. Kaulimbiu ya 2025 ni "Wanawake na Wasichana 2025: Kuimarisha Haki, Usawa na Uwezeshaji." Nchini Tanzania maadhimisho hayo yanaadhimishwa kitaifa mkoani Arusha, ambapo mgeni rasmi atakuwa Mh Dkt.Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.