
Ujumbe kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) ukiongozwa na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara Bibi Afia Sigge, ulipotembelea na kufanya majadiliano na Washauri Waandamizi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) jijini Dar es Salaam, Tanzania.

Jopo la TADB likiongozana na baadhi ya wanufaika wa benki hiyo walijadili mambo mbalimbali ikiwemo namna TADB inavyowezesha mageuzi ya kutoka katika kilimo cha mazoea kwenda kilimo cha biashara kwa msaada kutoka AfDB.

Aidha, Mshauri Mkuu wa AfDB alijifunza kuhusu TADB ikiwa ni pamoja na;
✅ Mamlaka ya TADB
✅ Utendaji wa TADB na
✅ Taarifa za utoaji wa mkopo wa TADB.
Walengwa wa TADB akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa Chanzo cha Mto Nile kutoka Misenyi mkoani Kagera Bw.Leodger Leonard na mfugaji wa kuku kutoka mkoa wa Pwani Bi.Jacqueline Tondi walipata fursa ya kueleza miradi yao na mikopo ya TADB iliwanufaisha.







