Rais Hussein Ali Mwinyi akitembelea banda la TADB katika Maonesho ya saba ya Kilimo “Nane Nane” 2024, Dole Kizimbani – Unguja.

Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Dk Hussein Ali Mwinyi, alitembelea banda hilo wakati akifungua rasmi maonesho ya saba ya Kilimo Zanzibar (Nane Nane) Agosti 3, 2024, Dole Kizimbani – Unguja.

Katika banda la TADB, HE. Dk.Mwinyi akipokelewa na Kaimu Meneja wa TADB Kanda ya Zanzibar Bw.Michael Madundo na kuelezwa majukumu ya benki ya kubadilisha kilimo nchini kutoka cha kujikimu kwenda cha kibiashara pamoja na maendeleo ya benki hiyo Zanzibar ikiwemo utoaji wa mikopo, idadi ya wanufaika wa mikopo ya benki na:

✅ Juhudi zinazofanywa na benki katika kutoa elimu na uhamasishaji wa masuala ya fedha na kilimo biashara Zanzibar

✅ Maendeleo ya mradi wa Ushirikiano wa Wasindikaji na Wazalishaji Tanzania (TI3P)

✅ Maendeleo ya Miradi ya Udhamini wa Mikopo kwa Wamiliki Wadogo (SCGS)

? Rais Mwinyi pia alipata fursa ya kuona kazi za wanufaika wa TADB, wakiwemo Kampuni ya Bin Mwewe (sekta ya kilimo cha bustani), Shemsa Taraba, na Kampuni ya MPF, (sekta ya kuku).