TADB kutoa mikopo ya hadi shilingi milioni 150 kwa watu binafsi na hadi shilingi milioni 500 kwa vikundi vya Wanawake na Vijana.

TADB imeidhinisha mikopo ya hadi bilioni 8 kwa wanawake na vijana katika kilimo

Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imezindua mpango maalum wa mikopo ya kilimo kwa wanawake na vijana unaolenga kukabiliana na changamoto za mitaji kwa kikundi kwa kulegeza baadhi ya vigezo na masharti ya mikopo ikiwemo kupunguza riba hadi asilimia 8.

✅Programu ya kuwakopesha wanawake na vijana Sh. 8 bilioni

✅Zaidi ya wanawake na vijana 25,000 kunufaika

✅ Riba kwa asilimia 8 pekee

Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw.Frank Nyabundege, amesema utekelezaji wa mikopo hiyo utaanza na kuwakopesha vijana wanufaika wa miradi na programu mbalimbali za vijana na wanawake ikiwemo mpango mpya uliozinduliwa -'Kujenga Kesho Bora' Youth Initiative for Agribusiness. BBT-YIA).

Ambapo TADB itatoa mikopo ya hadi shilingi milioni 150 kwa watu binafsi na hadi shilingi milioni 500 kwa vikundi na taasisi zinazoundwa na vikundi hivyo.

Programu hiyo ilizinduliwa Machi 21, 2023, mjini Dodoma ambapo mgeni rasmi wa hafla hiyo alikuwa ni Mheshimiwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Tulia Akson.