
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kupitia Mpango wake wa Udhamini wa Mikopo kwa Wakulima Wadogo (SCGS) na Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) wameweka mipango mkakati ya kuwawezesha wakulima wadogo visiwani humo.
Akizungumza wakati wa ziara ya kikazi PBZ, Meneja wa Mfuko wa Wakala wa TADB, Asha Tarimo, alisema kuwa PBZ ni washirika wa kimkakati katika kusambaza fedha za kilimo kwa wakulima wadogo katika kisiwa cha spice.

Bi.Tarimo aliongeza kuwa nia ya kuja Zanzibar ni kuwatembelea wakulima, kubaini changamoto zinazowakabili, kujadiliana na kujua njia bora za kuwapatia mikopo ya kilimo inayopatikana na nafuu kwa shughuli zao za kilimo, uvuvi na ufugaji.

Kupitia SCGS, hadi sasa TADB imetoa shilingi Bilioni 197 kwa wakulima wadogo wa Tanzania Bara na Zanzibar.



