TADB inaadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake

Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imeungana na maelfu ya wanawake duniani kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake #IWD Machi 8, 2023.

Mada ya mwaka huu ' DigitALL: Ubunifu na teknolojia kwa usawa wa kijinsia ' inayolenga kukumbusha jamii umuhimu wa kukuza uvumbuzi na teknolojia zinazozingatia jinsia na usawa.

Maadhimisho hayo yalihudhuriwa na mzungumzaji mgeni rasmi, Prof. Slyvia Temu, kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ambaye alizungumzia jinsi wafanyakazi wanawake na wanaume wanavyoweza kukumbatia usawa ndani na nje ya kazi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Frank Nyabundege, alitambua nafasi ya wanawake katika kuongeza thamani ya taasisi hiyo na kuhakikisha inaboresha uwakilishi wa wanawake katika nafasi za uongozi ndani ya benki hiyo.