TADB YASISITIZA UFUFUAJI WA VIWANDA HUONGEZA  TIJA,UZALISHAJI NA AJIRA KWA WAKULIMA WA PAMBA NA KAHAWA.Benki Ya Maendeleo Ya Kilimo (TADB) yakutana Na wadau wa pamba na kahawa mkoani Simiyu katika kubadilishana uzoefu katika warsha iliyohusisha wadau mbalimbali wa maendeleo ya kilimo, warsha hiyo iliyofanyika mkoani Simiyu ilifunguliwa na mkuu wa mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka, pamoja na wadau wa maendeleo yaani shirika la Huduma za Kifedha (FSDT) na Gatsby Foundation wakiwa waandalizi wakuu katika majadiliano hayo.

Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya maendeleo ya Kilimo, ndugu. Japhet Justine alieleza namna ambavyo benki ina mkakati ambao umelenga kufanya mapinduzi makubwa ya zao la pamba na kuwawezesha wakulima wa chini wa pamba pamoja na vyama vya ushirika (AMCOS) kuhakikisha kuwa wananufaika na kilimo cha pamba na na kuendelea kumiliki thamani ya zao mpaka linapofika kwa mlaji kutokana na ukuaji wa uzalishaji wa zao hilo ambapo Kwa mwaka 2017 pekee uzalishaji wa pamba ulikuwa tani 120,000, wakati kwa mwaka 2018 uzalishaji uliongezeka hadi zaidi ya 220,000.

TADB kwa kushirikiana na wadau wa zao la pamba wamependekeza kufanya mabadiliko ya zao hilo kwa kutumia mfumo wa mapinduzi uliyowezesha zao la kahawa mkoani Kagera, ambapo TADB iliwekeza Bilioni 23 Mwaka 2018 kama malipo ya awali kwa wakulima zaidi ya laki moja na elfu arobaini na mbili (242,000) na kufanikiwa kufufua viwanda vidogo vya kukoboa kahawa na kuajiri zaidi ya wafanyakazi 5,200.

Tunaamini kwa kutumia mfumo huu ambao ni endelevu kwa maendeleo ya wakulima wote, AMCOS na sekta nzima ya kilimo.