TADB NA ESRF ZAINGIA MAKUBALIANO YA KUWAJENGEA UWEZO WAKULIMA NCHINIBenki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) na Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na (ESRF) zimeingia makubaliano ya kufanya tafiti za maendeleo ya kilimo hasa katika kuwajengea uwezo wakulima wadogo nchini.Akizungumza wakati wa utiaji saini makubaliano hayo jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine amesema kuwa ushirikiano huo unalenga kuchagiza katika kuendeleza maeneo ya utafiti, uchambuzi wa sera na kuwajengea uwezo wakulima nchini ili kuweza kuharakisha mapinduzi ya kilimo Tanzania.

Akizungumzia malengo ya ushirikiano huo, Bw, Justine amesema pande zote zinalenga katika taasisi hizo zinalenga katika upatikanaji na uhamasishaji wa rasilimali fedha kwa ajili ya utafiti wa kilimo na maendeleo, uchambuzi wa sera, utetezi, na kujenga uwezo wa wakulima wadogo wadogo, wakulima wa kati na wakulima nchini Tanzania. Ameongeza kuwa ushirikiano huo utalenga katika kuandaa kanzi-data ya maarifa kwa ajili ya kujenga mtandao wa taarifa za kutosha kuhusu sekta ya kilimo ili kuwezesha maamuzi sahihi katika sera na utekelezaji wa masuala mbalimbali yanayohusiana na kilimo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa ESRF, Dk. Tausi Kida, amesema kuwa kuwa ushirikiano kati ya Benki ya Kilimo na Taasisi yake unalenga kufanya utafiti juu ya minyororo ya thamani ya kilimo pamoja na kuendeleza na kutekeleza mipango ya utetezi ili kusaidia katika utoaji wa maamuzi katika ngazi ya sera.