TADB yatoa mafunzo kwa wakulima wadogo wa michikichi Kigoma

Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imetoa mafunzo kwa wakulima wadogo zaidi ya 300 wa zao la mchikichi mkoani Kigoma.

Mafunzo hayo yalilenga wakulima katika:

✅Kilimo biashara ✅Elimu ya fedha ✅Usimamizi wa mikopo ✅Kanuni bora za mkopo

TADB imetoa zaidi ya Sh. bilioni 1.9 kuwezesha mnyororo wa thamani wa zao hilo.