IMG 1809

BENKI YA KILIMO YAKAGUA MIRADI YA KILIMO KILOMBERO

Katika kuhakikisha miradi inayopatiwa mikopo na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), uongozi wa Benki hiyo kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Bw. James Ihunyo wametembelea miradi minne iliyopo wilayani humo.
Miradi iliyotembelewa ni Kapolo AMCOS, Skimu ya Umwagiliaji ya Mkula. Nyingine ni Umoja wa Wakulima wa Miwa wa Msolwa Ujamaa na Hope ya Kidatu.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga alisema ameridhishwa na maendeleo ya miradi hiyo hali inayochochea ari ya Benki katika kutimiza lengo la Serikali la kukopesha wakulima nchini.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Bw. James Ihunyo aliwaasa wakulima hao kurudisha mikopo kwa wakati ili wakulima wengine waweze kupatiwa mikopo hiyo.
“Lengo la mikopo hiyo ni kuinua ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini nchini Tanzania, hivyo kuchelewesha mikopo hiyo kwa makusudi ni kurudisha nyuma juhudi hizi,” Bw. Ihunyo alisema.
Zaidi ya Shilingi bilioni 2 imekopeshwa kwa wakulima wa mpunga na miwa wilayani Kilombero.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *